“Kabla hatujafika Kigoma, Mheshimiwa Rais aliagiza watu kuja kutusapoti zaidi na kutushika mkono pale tunapokwama. Kama haitoshi yeye mwenyewe alikuwa akitazama shoo yetu hiyo live; sikutegemea kabisa.

Lakini tena akaamua kupiga simu on stage na kutupa moyo akiipongeza tasnia ya muziki na kuwatakia Watanzania heri ya mwaka mpya. Kwa kweli ni Rais wa kipekee sana na haijawahi kutokea." - Amesema hayo @diamondplatnumz juu ya sapoti aliyopata kutoka kwa mkuu wa nchi katika kuadhimisha miaka 10 toka aanze kufanya muziki wa Bongo Fleva.