Devenja Kibotuo mwenye umri wa miaka 35, Mkazi wa Kijiji cha Uchau Kusini Wilayani Moshi, Kilimanjaro anadaiwa kufukua kaburi la Mtoto wa Dada yake Juliana Andrea aliezikwa 2004 akiwa na miezi tisa, huku tukio hilo likihusishwa na imani za kishirikina.
_
Mama wa Marehemu amesema tukio limetokea January Mosi, 2020 ambapo walimkuta Devenja amefukua kaburi huku mabaki ya mifupa na sanda vikiwa juu na akaotesha mgomba kwenye eneo la kaburi.
_
"Tunamshikilia Devenja kwa kufukua kaburi bila ya kuwa na kibali cha Mahakama, tutashirikisha idara ya Afya kujua kama ana akili timamu kabla ya kuchukua hatua" - POLISI KILIMANJARO