Staa wa BongoFleva Ommy Dimpoz, amefunguka kuwa yeye sio mtu wa kuweka mahusiano yake wazi, pia hana matatizo yoyote na mastaa wa kike Bongo, japokuwa huwa haonekani akiwa nao karibu.


Ommy Dimpoz akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, amesema ana maisha yake ya kawaida na binafsi na kwamba hana chuki na wanawake wa Bongo.

"Nafikiri kuna maisha binafsi na maisha ya kawaida, kuna muda kama msanii unahitaji maisha yako binafsi, halafu mimi sio mtu wa mahusiano yangu kuyaweka wazi, nina upendo wa kutosha na wanawake wote wa Bongo kwa hiyo sina tatizo nao wala siwachukii" amesema Ommy Dimpoz.

Akizungumzia kuhusu kutoonekana akiwa nao karibu na wanawake mastaa Ommy Dimpoz ameeleza kuwa, "Karibia wote ni marafiki zangu na tunashirikiana kwenye mambo mengi, nafikiri ukaribu sio lazima tuwe nao mitandaoni na mimi sijaweka sana kwenye mitandao, lakini tupo poa na vizuri kabisa" ameongeza.TOP STORIES

CURRENT AFFAIRS
RC Mbeya awatimua Kidato cha 5 na 6 awataka kurudi

ENTERTAINMENT
Seyi Shay ataja orodha ya wanaume alio-date nao

CURRENT AFFAIRS
Kama alivyosema Makonda ''Wameoga'' - Kamwelwe

CURRENT AFFAIRS
CHADEMA yatoa maagizo matatu kuhusu Halima Mdee


MOST POPULAR

CURRENT AFFAIRS
Sabaya arejesha eneo liliporwa na Kapteni Mstaafu

ENTERTAINMENT
'Sikijui cheo cha Job Ndugai' - Shamsa Ford

CURRENT AFFAIRS
'Mlionipigia kura, hazikutosha' - John Heche

CURRENT AFFAIRS
Mzee mwenye watoto 60, wajukuu 70 afungua Shule

SPORT
Frank Domayo apelekwa South Afrika kutibiwa
ABOUT US
ABOUT USADVERTISEJOBSTERMS & CONDITIONSCONTACT USFREQUENTLY ASKED QUESTIONS
NETWORK
IPP MEDIAEAST AFRICA RADIOITVRADIO ONECAPITAL RADIOLOKOPROMO
© 2019 East Africa Television Limited. All Rights Reserved