Kupitia EATV & EA Radio Digital, msanii Baraka The Prince amesema kuna wasanii wengi wanaotukana sana akiwemo Nay wa Mitego, lakini pia kuna wengine wana matusi mabaya kuliko hata yeye.


Baraka The Prince amesema hayo baada ya kutajwa na mashabiki kama ndiyo msanii, anayeongoza kutukana watu katika mtandao wa Instagram, ambapo amesema mara nyingi hufanya hivyo ikitokea mtu amemkera.

"Mlishakariri hivyo kama ni Baraka tu kuna wengine hata hamuwafuatilii, wanatukana na wana matusi mabaya kuliko mimi, mimi namfikia Nay Wa Mitego kutukana, pia kuna muda wasanii kibao wanatukana lakini likitokeaga kwangu hata kama ni moja watu wanalichukua" ameeleza Baraka The Prince.

Aidha msanii huyo ameendelea kusema

"Mimi siyo kama nashindwa kuizuia mihemko yangu ila naishi ndani ya hisia zangu kwa sababu zinafanya niwe huru na amani, ukinikera nakuchana, hutakiwi kukaa na kinyongo mtu akizingua pita naye na kama matusi yatafanya hata tusiheshimiane ni sawa tutakwenda hivyo" ameongeza.