INADAIWA mitandaoni kwamba, kati ya wanawake wanaojua kupaniki, basi mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ anaweza kuwa kwenye kumi bora.  Inavyoonekana Zari ambaye ni mjasiriamali kutoka nchini Uganda, mwenye makazi yake jijini Pretoria, Afrika Kusini, hayupo vizuri baada ya juzi kumbwatukia mmoja wa wafuasi wake mtandaoni.

Zari ambaye ni mzazi mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alimwambia mfuasi wake huyo kwamba, yule aliyedai ni mumewe aliyefunga naye ndoa miezi kadhaa iliyopita, King Bae au Mr M, eti amekufa.

Zari ambaye ni mama wa watoto watano, alijikuta akitoa kauli hiyo baada ya mfuasi wake huyo kumuuliza mbona siku hizi King Bae haonekani? “Amekufa.” Zari alimjibu kwa kifupi. Majibu ya Zari yanaonekana kama alikuwa anatania, lakini baadhi ya wachangiaji kwenye ukurasa wake wa Instagram walihitimisha kwamba, kuna kitu hakijakaa sawa kwenye suala zima la uhusiano wa kimapenzi kwa Zari.

Baadhi ya watu walikwenda mbali na kudai kwamba, eti hakukuwa na King Bae, bali ilikuwa ni zuga tu baada ya kuachana na Diamond au Mondi ili naye aonekane wanaume wanamtaka. Wengine walidai kuwa, huenda alikuwepo mwanaume huyo, lakini sasa wameachana. Pamoja na kujulikana kuwa ana mwanaume aliyemtambulisha kwa jina hilo, lakini hakuwahi kumfunua au kumuonesha uso kwa madai ya kwamba anahofia nyakunyaku wa mjini watamuibia