ABIRIA  wawili waliokuwa wanasafiri na basi la kampuni ya Buti la Zungu kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Mtwara wamenusurika kifo baada ya kupewa biskuti zinazodhaniwa kuwa na dawa za kulevya na wakaibiwa.


Abiria hao ambao ni Dadi Rashid, Ofisa Elimu Taaluma wilayani Rufiji,  na Omary Burian ambaye ni mfanyakazi wa Bodi ya Korosho Dar es Salaam, wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi