KILA mtu anapenda kujisifia sehemu mbalimbali za mwili wake, ushawahi kujiuliza aliyekuwa mtangazaji matata wa stesheni mbalimbali za redio, Penieli Mungilwa ‘Penny’ anapenda kujisifia nini? Basi mtangazaji huyo anasema sura yake nzuri ndiyo kitu pekee kinachomfanya asizeeke mapema.Akipiga pang’ang’a Za Motomoto ya Risasi, Penny alisema kwa sasa anakiri usemi wa watu wengi kuwa unavyozidi kuwa mtu mzima, ndipo unakuwa mzuri na mrembo.“Huwa najiangalia kwenye kioo mara kwa mara, kuna wakati siamini maana nakuwa mzuri siku hadi siku mpaka sijiamini lakini sina shaka, nilishawahi kuambiwa kuwa ukiwa unazeeka ndivyo unazidi kuwa mzuri siku hadi siku. Hivyo, sura yangu kuja kuwa na makunyanzi itachukua muda sana,” alisema Penny ambaye kwa sasa amegeukia mapishi