KWELI mambo hubadilika! Umemsikia mwigizaji wa kitambo kwenye tamthiliya za Kibongo, Nuru Nassoro ‘Nora’? Nora ameliambia Amani kuwa, aliwahi kuchoma nguo zote ambazo hazikuwa na maadili na za kumpendeza Mungu ikiwemo vimini.  Nora amesema, baada ya kumjua Mungu kiundani, aliamua kutoa vitu vyote alivyokuwa navyo ambavyo vilikuwa chukizo kwa dini yake ya Kiislam.

“Nilichoma mpaka nguo zangu ambazo niliona wazi nilikuwa navaa na hazikuwa sahihi kabisa kwa Mwenyezi Mungu maana sasa nimekuwa mpya na sitaki hata kukumbuka kama nilicheza filamu zisizo na maadili,” alisema Nora.