Muigizaji na mfanyabiashara hapa nchini, Shamsa Ford, amesema kwenye suala la umbea mara nyingi hupendelea umbea wa moto moto na si ule unaotokea kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram.Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Shamsa Ford amesema mara nyingi akaapo na muigizaji mwenzake Aunty Ezekiel, huwa wanapenda kupiga umbea wa masuala yanayoendelea mjini na kwamba Wema Sepetu ndiye anayeongoza kwa kusema wenzake.

"Nikikaaga na Aunty tunachekaga tu mambo ya mjini yanayoendelea, tukiona watu wametendwa tunacheka na tunawateta ila muda mwingi ni vitu vya kuchekeshachekesha, ila hatutabiriki hata mtu akija akigeuza kisogo kidogo tu tunamsema, lakini Wema Sepetu ndiyo wa kwanza anayeongoza kusema wenzie"amesema Shamsa Ford.