WATU wasiojulikana wamemteka Shelton Lalgy, mtoto wa mfanyabiashara mkubwa nchini Msumbiji, Juneide Lalgy.Tukio hilo limetokea jijini Matola jana Alhamisi, Novemba 28, 2019, asubuhi wakati Shelton akirejea nyumbani kutoka mazoezini (gym). Watekaji walimuingiza ndani ya gari aina ya Toyota Noah lenye rangi nyeupe na kutoweka naye kusikojulikana.Taarifa ya polisi imesema wanalifanyia uchunguzi tukio hilo ili kupata uhalisia wake.  Tukio hilo limetokea wakati wimbi la utekaji lilikuwa limepungua kwa kiasi kikubwa katika miji ya Maputo na Matola.Kampuni ya  Transportes Lalgy, iliyoanza shughuli zake mnamo miaka ya 1980 ni moja ya makampuni makubwa ya usafirishaji nchini Msumbiji ambalo hufika katika baadhi ya nchi nyingine za kusini mwa Afrika, likiwa na makao yake makuu jijini Matola, mkoani Maputo.