Baada ya staa wa filamu, Irene Uwoya kuweka picha kwenye ukurasa wake wa Instagram inayomuonesha tumbo lake likiwa kawaida tofauti na siku zilizopita alivyojianika kuwa ana ujauzito huku ukiwa umeonekana, mimba yake imepewa jina la upepo wa kisulisuli.Wadau mbalimbali kwenye mtandao huo walijikuta wakizungumza kila mmoja kivyake huku wakisema kuwa mimba ya mrembo huyo ni upepo wa kisulisuli kwani ni hivi karibuni tu alionekana akiwa na tumbo kubwa lakini ghafla limeyeyuka.“Yaani hawa wasanii wetu hawa wana mambo mengi sana sijui hata mimba zao huwa zinaendaga wapi, maana huyu juzi tu alionekana tumbo likiwa limeanza kuwa kubwa lakini leo yuko flat kabisa,” aliandika mmoja wa wafuasi wa Uwoya huku akiambatanisha na picha.