MAMBO ni moto! Unaambiwa huko Ista, Idris kalianzisha kwa kumsema maneno Madam Wema Sepetu sasa alichokipata ni zaidi ya matusi.Kwenye ukurasa wake wa Insta, Idris aliandika maneno ambayo hakumtaja Madam lakini wananzengo wakajua kabisa anamaanisha kumlenga mrembo huyo ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake ndipo walipoanza kumchamba.Idris aliandika hivi: “Najua ni asubuhi ila nikiona selebriti mwingine aliyekonda kwa stress au kukosa hela ya kula halafu anakuja kututangazia dawa za kupunguza unene wakati hata hazijui wala hazitumii, hazifanyi kazi, najitolea kumnyonga.” Baada ya kuweka ujumbe huo, Idris alikula matusi kibao ambayo kimsingi hayafai kuandikwa hapa