JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limefanikiwa kuua watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi sugu akiwemo aliyefahamika kwa jina la Kambare ambaye alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na jeshi hilo.Hayo yamesemwa leo Jumatano, Novemba 6, 2019 na kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mkutano wa SADC unaotarajiwa kuanza keshokutwa, Novemba 8, katika Ukumbi wa Kimatataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.