MKALI muziki wa Taarab Bongo, Isha Ramadhani maarufu kama Isha Mashauzi amefunguka kuwa wasanii wengi nchini hawajui thamani yao mbele ya mashabiki.Akipiga stori na Jahazi la Pwani kinachorushwa kila Jumapili, saa 10 mpaka 12 jioni ndani ya +255Global Radio, Isha amesema kumekuwa na wimbi kubwa la wasanii hasa wa Taarab kufanya shoo za bure na mara nyingine unakuta kiingilio ni kinywaji jambo ambalo linamuumiza msanii mwenyewe kwani nguvu yote aliyoitumia kwenye maandalizi inakuwa ni kazi bure.“Yaani mimi kwanza nikimkuta mtu yeyote au bendi yoyote inatumia wimbo wangu kwenye shoo ya bure hatutaelewana, kwanza inakuwa hainipi heshima mimi kama msanii kwa sababu nimetumia muda mwingi kuandaa kazi hiyo halikadhalika nimetumia gharama kuandaa kazi hiyo hivyo basi kazi yangu itakuwa ni sawa na bure yani naambulia maumivu,” alisema Isha.Isha alikazia kwa kutolea mfano wasanii wa muziki wa Bongo Fleva kuwa hakuna hata mmoja wao ambaye alishawahi kusikika anafanya shoo ya bure kwa sababu wao walishatambua thamani yao kwa jamii. Isha kwa sasa anatamba na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Kisosora’.Ili kusikiliza +255Global Radio nenda kwenye Google Playstore kama unatumia Android au kama ni mtumiaji wa iOS ingia kwenye AppStore kisha andika +255Global Radio na upakue App hiyo ili uendelee kufurahia ulimwengu wa habari kiganjani mwako.