MJINI kuna mambo! Sikia hii ya msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ambaye amesema atamnyonyoa nywele msichana aliyejipachika jina la Beyonce wa Bongo ambaye ni mpenzi wa mwigizaji Yusuf Mlela.  Beyonce ni yule mrembo ambaye juzikati alizua varangati hotelini na mchekeshaji Ebitoke hadi akavuliwa wigi, kisa penzi la Mlela.

Gigy ameliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, yeye hatamvua tu wigi, bali atamtoa nywele kwa mikono, maana anaona kama anampanda kichwani. “Huyo msichana ananichokoza, lakini hajui moto wangu. Mimi sitamvua wigi, bali nitamnyonyoa nywele,” alisema Gigy bila kueleza chanzo cha ugomvi wao.