CAG mpya Charles Kichere akipokea Ofisi leo November 5, 2019 “Nitashirikiana na wenzangu tutajenga timuProfesa usiwe na wasiwasi tutajenga timu nzuri nitahakikisha kuanzia chini tunakua na timu yenye uwezo wa fanya kazi, kwa sababu watu mkisambaratika sambaratika hapo utakua umesambaratisha Taasisi na hutafurahi kuona Mwanafunzi wako anaisambaratisha Taasisi ambayo ulikuwepo kwa miaka mitano”

“Kama kutakua na mabadiliko yatafanyika kwa umakini mkubwa, naenda kufanya kazi kulinda mapato na nitalinda, sitakua na aibu kwa watu wanaotumia mapato ya Serikali vibaya nitawaripoti” CAG mpya Kichere