Mfalme wa muziki nchini Tanzania, Ali Kiba akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuelekea mkoani Tabora kwenye 'tour' yake, amekutana na wachezaji wa timu ya Soka ya Yanga na kusalimiana nao, wakati wenyewe wakielekea mkoani Mwanza

kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Alliance FC ya jijini humo.

Katika safari hiyo Alikiba ameongozana na timu ya watu mbalimbali, kutoka kituo cha East Africa TV na East Africa Radio, kwa ajili ya maandalizi ya Tamasha lake la #AliKibaUnforgettableTour ambalo anatarajia kulifanya siku ya Jumamosi ya Novemba 29, 2019 mkoani Tabora.

Akiwa mkoani Tabora, Ali Kiba atafaya shughuli mbalimbali ikiwemo kuzungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ardhi mkoani humo na kuhamasisha upimaji wa magonjwa bure kwa mashabiki zake mkoani humo na Mikoa ya jirani.

Aidha akiwa mkoani humo Ali Kiba anatarajiwa kufanya Tamasha maalum la Muziki, siku ya Novemba 29, ikiwa ni kuadhimisha kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.

Tazama video hapo chini uone alichokifanya Ali Kiba alipokutana na wachezaji wa Yanga.