MWANADADA aliyewahi kuwa mwigizaji na mtangazaji kwenye vituo mbalimbali vya redio na televisheni Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ amesema kama yeye ameamua kuacha mambo ya kujirusha hovyo na kusababisha matukio kadha wa kadha yasiyo na staha (uwaluwalu), wengine wao ni kina nani hadi wasiache?Akizungumza na Amani, Lulu amesema kuna wakati unafika inabidi mtu aache mambo hayo kwa sababu mtu anaamua kubadilisha maisha na kuwa mtu mwingine kabisa.“Nashangaa kuna watu hadi sasa wanasema kuwa hawawezi kuishi bila kunywa pombe au kutoka kwenda klabu, lakini kumbe maisha yamebadilika ndiyo maana ninawaambia maduu wenzangu, kama mimi nimeyaweka kando hayo yote wao ni kina nani wasibadilike na kumjua Mungu zaidi,” alisema Aunty Lulu ambaye sasa hivi anatumia muda mwingi kuwa kanisani na kufanya shughuli za kiroho zaidi.