Kunako 1995 Diamond Platnumz alianza elimu ya Nursery katika shule ya Chakula Bora iliyopo Tandale Uzuri hadi alipomaliza na kujiunga na Elimu ya Msingi yaani (Primary School) mwaka 1996 katika shule ya msingi Tandale magharibi iliyopo jijin Dar-es-salaam. .

Ilipofika mwaka 2000 akiwa darasa la tano diamond alionekana kuanza kupenda sana muziki, hivyo alianza kucopy baadhi ya na kukrem nyimbo za wasanii waliokuwa wakihit ndani na nje ya nchi kwa kipindi hicho na kuwa anaimba katika sehem tofautitofauti.

Mara nyingi mama yake alikuwa akimnunulia kanda za album za wasanii tofauti waliokuwa wakihit kipindi hicho na hata kumuandikia baadhi ya nyimbo za wasanii hao ili mwanae aweze kuzishika na kuimba kirahisi, na wakati mwingine hata kumpeleka katika matamasha tofautitofauti ya tallent show ili mwanae apate nafasi ya kuimba, kitu ambacho baadhi ya ndugu wa familia waliona ni kama kumpotosha na kumuharibu mtoto huyo badala ya kumuhimiza kimasomo. .

Lakini miaka mingi baadaye kwasasa Diamond amefanikiwa kupitia muziki, kutoa ajira nyingi na fursa mbalimbali Kwa watu wengine na ndie anaelezwa kuwa msanii mwenye ushawishi mkubwa zaidi toka Tanzania