Mwanariadha aliyejizolea umaarufu duniani kutoka nchini Kenya, Eliud Kipchoge amekitaka kituo cha Radio cha NRG cha nchini humo, Kuacha mara moja kutumia jina lake kibiashara ikiwemo kuomba Followers kwenye mtandao wa Instagram.


Eliud Kipchoge amekituhumu kituo hicho kupitia barua aliyoiandika mwanasheria wake, Ambapo amesema kituo hicho kinaendesha #KipchogeChallenge kwenye mtandao wa Instagram na kuwaomba watumiaji wa mtandao huo wa-Follow akaunti yao ya Instagram na ikifikisha wafuasi milioni 1,  Watampatia  Eliud Kipchoge gari la kisasa aina ya BMW i8.


Barua hiyo imeeleza kuwa mpaka sasa tovuti ya Radio imebadilisha bila hata makubaliano na inatumia anwani ya ilove.kipchoge.radio na kuweka picha yake kinyume kabisa na matakwa yake.

Kampeni ya kuomba followers mitandaoni ilikuwa inaendeshwa na mchekeshaji maarufu nchini humo, Eric Omondi.

Barua hiyo ya onyo imeutaka uongozi wa kituo hicho pendwa kwa burudani kifute posti zote kwenye mitandao yao ya kijamii na kwenye website ndani ya masaa mawili la sivyo atawaburuza mahakamani.

Wadau wengi wa burudani nchini humo, Kupitia mitandao ya kijamii wamekilaumu kituo hicho kwa kutumia jina la mwanariadha huyo bila makubaliano ya kibiashara. Soma barua hiyo hapa chini