MPENZI wa staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Tanasha Donna, amezima tetesi za kudanganya tarehe ya kuzaliwa kwa mtoto wao zilizosambaa katika mitandao ya kijamii hivi karibuni.

baada ya Diamond Platnumz kutangaza kuwa amebahatika kupata mtoto wa kiume na mpenzi wake Tanasha katika tarehe ambayo na yeye amezaliwa, baadhi ya mashabiki walimjia juu na kutaka aache kudanganya watu kwani inaonyesha mtoto alizaliwa siku kadhaa zilizopita.

Katika kuweka sawa, Tanasha alitumia Insta Stories kuweka kibandiko maalum cha hospitali ya Aga Khan alichovishwa mkononi kinaonyesha mtoto wake amezaliwa Oktoba 2, mwaka huu na namba ya kuzaliwa ni 158-03-1. “Nimekaa leba kwa saa 17 na ujauzito wangu umedumu kwa wiki 42 na nimejifungua kwa njia ya kawaida, sasa ni mama wa mtoto mzuri wa kiume anayeshea ‘birthday’ na mpenzi wangu (Diamond),” aliandika Tanasha