Staa wa Bongofleva na Boss Fyn by Falsafa Hamis Mwinjuma maarufu kama MwanaFA ameweka rekodi mpya baada ya kufanikiwa kufika Kilele cha Uhuru Cha Mlima Kilimanjaro na kuwa msanii wa kwanza Tanzania kufika kileleni miongoni mwa walioshiriki kampeni iliyoandaliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla.

MwanaFA pamoja na wasanii wengine wa muziki wa kizazi kipya na Bongo Movies wameshiriki katika challenge ya kupanda Mlima huo ikipewa jina la HK Kilimanjaro Challenge 2019.