Muigizaji wa filamu nchini Dorrah amesema moja ya wasanii ambao hawezi kutoka nao muigizaji Pierre Likwidi, na kusema bila ulevi huenda msanii huyo asingeingia kabisa kwenye sanaa.


Dorah ametoa kauli hiyo wakai akizungumza kwenye kipindi cha Kikaangoni kinachorushwa na kupiia kurasa za Facebook na YouTube ya East Africa TV, ambapo amnesema moja ya wasanii ambao wanafosi kuigiza ni Piere.

"Kiukweli ukiniuliza ni Msanii gani kwenye sanaa hawezi kuigiza nitashinwa ila ukishakuwa Msanii unaweza kuigiza, ila katika watu ambao hawawezi kuigiza ni Pierre, usingekuwa ulevi asingeingia kwenye maigizo" amesema Dorah

Aidha kuhusiana na suala la mahusiano msanii amesema hawezi hata kidogo kutoka na Piere kuokana na tabia yake ya ulevi.

"Mpenzi wangu ni mrefu, mtu mfupi kama Pierre hapana, kwanza mlevi sana na mimi sipendi mwanaume anayelewa'amesema Dorah