Jeneza la miaka 2,100 lililokuwa limeibiwa kutoka Misri kwa kutumia leseni bandia, la kuhani wa zamani wa Misri Nedjemankh lilirudishwa katika jumba la makumbusho la Misri siku ya Jumatano.

Jeneza hilo lilipatikana kwenye Jumba la Sanaa la Metropolitan, New York baada ya kununuliwa kutoka kwa muuzaji wa sanaa mjini Paris mwaka wa 2017 kwa dola milioni nne za Marekani. Marekani imeomba Misri msamaha.