Mdau kutoka JamiiForums anasema kwa uchunguzi alioufanya amegundua mambo ya hovyo yana mashabiki wengi kuliko mambo ya maana

Anasema mtu akiandika habari za udaku na ujinga anapata michango mingi kutoka kwa jamii kuliko mtu aliyechambua mambo makubwa ya kitaifa yenye hata kurasa moja

Anaongeza kwa kueleza kuwa Watanzania wapo tayari kusoma mistari miwili hata kama haina faida kwao na kuchangia mada na wakaacha kusoma mistari 100 yenye maudhui ya kuwajenga kwa dhana kwamba wanapoteza muda

Maoni yako ni yapi katika hili?