Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekanusha taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kwamba Waziri Ummy Mwalimu amezindua duka linalosifika kwa kuuza ’Dawa za kukuza nyeti za kiume’ hapa Tanzania, Wizara imesema Waziri Ummy hajawahi kufika na hata kulifahamu duka hilo.