Msanii mkongwe kwenye gemu ya muziki wa Bongo Fleva, Domo Kaya ambaye ameshawahi kutamba na nyimbo ya 'Dingi' amefunguka kuwa hana tatizo na Alikba kwenye swala zima la kutumia msemo wake ya YeBaba ambao yeye alikuwa anautumia miaka mingi huko nyuma.

Akizungumza kwenye moja ya Interview Domo Kaya amesema "Ule ni msemo wangu ila kwangu sina tatzio kwa Kiba kuutumia na wala sijamkataza kutumia licha ya kuwa ni msemo wangu wa miaka mingi"

Kwa upande mwingine Domo amewataka Mashabiki zake kutotumia kauli kuwa Kiba ameiba usemi huo wa Yebaba.