Katika mitandao yote ya kijamii siku ya jana na leo, ilitrend taarifa moja ambayo ilimuhusisha muigizaji Menina, katika picha na video za faragha.

EATV & EA Radio Digital, imemdaka  msanii wa Bongofleva Barakah The Prince, ambaye amefunguka suala la kujirekodi video na picha akiwa faragha na mpenzi wake Naj Dattani.

"Haiwezi ikatokea hicho kitu, hata tukiwa tumeeachana kwa sababu mimi na yeye hatujawahi kuwa na mazoea hayo, halafu Najma namchukulia kama mke wangu, sina ujasiri wa kumuomba tujirekodi picha au video zisizo na maadili, siku zote mwanaume anayejitambua na anayejiheshimu hawezi kumuomba mpenzi wake mjirekodi wakati mkiwa faragha"amesema Baraka.

Baraka ameongeza kuwa mwanaume ndiyo huanza kuomba kujirekodi ila mwanamke hawezi kufanya hivyo hata siku moja, kwa hiyo ukifanya kitu kama hicho, unamchukulia mpenzi wako kama huna mipango naye.

Pia Barakah The Prince amesema sasa hivi anajua ana maadui wengi sana wanaomchukia, ambao kwa namna moja au nyingine wanamkwamisha kuendelea kimuziki na mipango yake.

VIDEO: