Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amezindua ATM ya kwanza ya Maziwa Nchini katika mji wa Moshi yenye uwezo wa kutoa maziwa kulingana na kiwango chako cha fedha

Unaweza kupata maziwa kuanzia kwa Tsh. 50, 100, 400, 600, 1000, 2000, na kuendelea

Mradi huu umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya na Kusimamiwa na SNV pamoja na Match Maker Associates ambapo wameweza kujenga ATM 3 za kuuza Maziwa

ATM zingine zipo Wilaya ya Hai na nyingine ipo Mjini Arusha. Sambamba na hili, RC amezindua Jukwaa la Ubunifu la Maziwa Mkoani humo na amekubali kuwa mlezi wa Jukwaa hilo