UONGOZI wa Yanga umesema kuwa unajipanga kufanya vema kwenye michuano ya kimataifa inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) ili kufikia hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na kuvuna mkwanja mrefu.

Yanga itamenyana na Zesco Septemba 14 uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa hatua ya kwanza kabla ya kutinga hatua ya makundi.

Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa hesabu kubwa ni kuona kikosi kinafanya makubwa ili kupata fedha kwa ajili ya matumizi ya klabu.

"Timu ikishinda na kupenya hatua  ya makundi kuna fedha ambazo timu itapata tena ni nyigi hapo itakuwa rahisi kwetu kuziweka kwenye matumizi yetu ya timu.

"Kila kitu kinawezekana ukizingatia kwamba tuna kikosi kipana na kilicho imara, mashabiki watupe sapoti ili tufikie malengo yetu," amesema.