KUMBE kuna wakati unafika binadamu anasahau alikotoka? Msikie mwigizaji wa kitambo Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’, eti amesahau kabisa kama alishawahi kuwa staa wa sinema Bongo.

Nora ameliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, kwa sasa amebadilika kiakili hivyo hakumbuki kama alishawahi kuwa msanii kwani ni ishu ambayo hataki kabisa kuisikia kwa kuwa hivi sasa ameamua kumrudia Mungu mazima.

“Kuna vingine mtu hutamani hata kuvisikia maana vingi vilikuwa dhambi. Kichwani kwangu imeshafutika kabisa kama niliwahi kuwa staa wa sinema,” alisema Nora ambaye kwa sasa anafundisha maadili ya Dini ya Kiislam kama ilivyo kwa Mzee Yusuf aliyekuwa staa wa muziki wa Taarab nchini

STORI: IMELDA MTEMA,DAR