Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania, Tundu Lissu, amebadili tarehe yake ya kuja nchini baada ya kuarifiwa kuwa daktari wake kusema anataka kumuona Oktoba 1 mwaka huu.

Kipindi cha nyuma Lissu alidokeza kuwa atarudi Septemba 7 ambayo itakuwa ni Jumamosi ya wiki hii, hata hivyo Lissu sasa anasema bado anasubiri kupata ridhaa ya madaktari wake iwapo anaweza kurudi nyumbani.

"Nilisema mwanzoni kwamba nitarudi tarehe 7 septemba ya mwaka huu ambayo ni Jumamosi ya keshokutwa lakini mpaka sasa hivi sijapata ruhusa ya madaktari wangu, dakari wangu ameniambia ataniona tarehe 1 Oktoba na kwa mara ya mwisho ataniona tarehe 8 Oktoba," amesema Lissu.

"Kwahiyo hii tarehe ya mwisho ya 7 Oktoba haitawezekena kwasababu daktari wangu anahitaji kuniona kwenye hizo tarehe 2 baada ya hapo ntafanya utaratibu wa kurudi nyumbani."

 Septemba 7 ni miaka miwili tangu Lissu kushambuliwa na watu wasiojulikana huko Jijini Dodoma.