Beki wa kulia wa Klabu ya Yanga, Juma Abdul Jaffar Mnyamani amepata pigo kubwa baada ya kuondokewa na mama yake mzazi ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Septemba 5, 2019.

Nahodha huyo msaidizi wa Yanga amepata taarifa za msiba wa mama yake asubuhi ya leo akiwa kambini jijini Mwanza akijiandaa kwenda mazoezini. Abdul anatarajia kuondoka jioni ya leo kurejea Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Klabu ya Yanga imeandika;

Uongozi wa Klabu ya Yanga SC kwa niamba ya Wanachama na wapenzi wa Yanga unatoa pole kwa mchezaji wetu Juma Adul kwa msiba wa kufiwa na Mama yake Mzazi. Yanga tuko pamoja naye katika kipindi hiki kigumu cha Majonzi. Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema Peponi. Amina.

Taratibu za msiba tutawajuza baadaye.