Ndege ya kijeshi iliyoanguka kaskazini magharibi
mwa Ufaransa, ilipekea rubani mmoja kuruka na kuangukia katika nyaya za umeme.

Baada ya ndege hiyo kupata hitilafu angani marubani wote waliruka katika ndege hiyo katika eneo la Brittany

Rubani aliyeangukia umeme, anaendelea vizuri na alinusurika kupigwa shoti ya umeme. Nyaya za umeme ambazo mtu yule aliziangukia zilikuwa na nguvu za volti 250,000

Vyombo vya habari vya Ufaransa vimeonyesha picha ya namna parachuti ilivyokuwa inashuka karibu na nyaya za umeme, huku ikielezwa kuwa Ndege hiyo ya jeshi inaripotiwa kuwa haikuwa imebeba silaha.