Kundi la Rostam linaloundwa na Roma & Stamina, wamepiga stori na kipindi cha "Friday Night Live" ya East Africa Television na kufunguka kuwa Billnass anapenda sana mapenzi.

Rostam wamefunguka hayo baada ya kusambaa kwa video katika mtandao wa kijamii wa Instagram ikiwaonyesha wakimzungumzia Billnass kuendekeza mapenzi.

"Ni mdogo wangu ila ni ukweli kabisa, unajua hata sasa hivi waandaji wa show hawampigii simu Nenga 'Billnass' kumtaka kwenye show, huwa wanampigia Nandy na wanajua kabisa Billnass atamfuata nyuma kama sanamu" ameleeza Roma.

Billnass na Nandy wamekuwa wanatajwa sana siku za hivi karibuni kuwa wamerudiana japokuwa wenyewe wamekuwa wakikanusha kwenye baadhi ya mahojiano wanayofanya kwenye vyombo mbalimbali vya habari.

Aidha Roma na Stamina "Rostam" wameachia wimbo wao Audio na Video unaoitwa Kijewe Nongwa waliomshirikisha Nay Wa Mitego.