Cyril Ramaphosa Rais wa Afrika kusini ameomba msamaha kwa rais wa Nigeria Muhammadu Buhari na wanigeria wote walioathirika na machafuko dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini.Kupitia kwa mjumbe wake Jeff Radebe, Ramaphosa amesema tayari nchi yake imeweka mikakati dhabiti ilikuzuia kutokea tena kwa vitendo hivyo vya chuki.

Si Nigeria pekee kwani Ramaphosa ametuma timu ya wawakilishi wake katika nchi saba za Afrika kupeleka salamu za umoja na ushirikiano kutokana na machafuko dhidi ya wageni nchini mwake.