MMOJA wa warembo wanaotikisa kwenye mitandao ya kijamii (socialite) Bongo, Jacqueline Obeid ‘Poshy Queen’ ametoa povu kuhusu skendo inayomuandama ya kuongeza kalio. Katika mahojiano maalum na Gazeti la Ijumaa Wikienda juu ya ishu hiyo, Poshy anasema anachukia mno anapoambiwa ameongeza makalio na kutengeneza shepu, jambo ambalo hafikirii kulifanya na


kama mtu anadhani ni ishu rahisi, basi naye akafanye. “Kwa nini nifanye hivyo? Kama mtu alishawahi kumuona mama yangu alivyo, asingekurupuka kusema,” anasema Poshy