Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa alipowaita Watendaji Kata Ikulu wengine hawakufurahi.

Rais Magufuli pia amesema anajua kuwa Maboss wao hawawezi kufurahi ila yeye ndio Boss Mkubwa.

"Nilipowaita wengine hawakufurahia, Rais anawaita hadi watendaji Kata Ikulu?, nasikia wa Kyerwa wamepewa Laki na 50 kuja Dar Es Salaam wakati wa Dodoma wameletwa na basi maalum, haiwezekani fulani apate urahisi, mwingine apate tabu, Mabosi wenu hawawezi kufurahia ila mimi ni Boss Mkubwa,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Watendaji wa Kata katika Mamlaka ya Serikali za kata zote Tanzania Bara katika Bustani za Ukumbi wa Kikwete Ikulu Jijini Dar es salaam.