"My brother Ali Kiba..! Katika kuachwa au kuachana kinachoumiza sio kumpoteza tu yule mtu uliempenda...huyo mtu unaweza ukamuacha akaenda tu. Kinachouma sana ni muda uliopoteza, emotional wastage na muda mwingine hata gharama uliyotumia ili kumfanya aonekane bora...pia kupoteza lile tumaini kwamba mambo yatakua sawa na namna ambavyo utawaambia rafiki zako na ndugu zako ambao walikuwa wakimfahamu kwamba hakuna mahusiano tena. Hiko ndicho kinachouma zaidi.

Unapomuumiza mtu na ukamuona analia, usifikiri anakulilia wewe. Wanalia kwa sababu wamepoteza muda wao wa thamani kwa mtu ambae hata hakustahili kupewa huo muda..." Volumu Ipo sawa?" Amesema Mwinjaku