Aliyewahikuwa Bodygurd wa Diamond Platnumz Mwarabu Fighter amefunguka mengi kuhusu maisha yake ya sasa na yale maisha aliyoishi wakati akifanya akzi na Diamond Platnumz.Akipiga stori na Bongo5 Mwarabu Fighter amesema kuwa:- ” Nilipoancha kazi nilihangaika sana maana sikuwa na hata sent mia, mke wangu aliuza genge mtaani ili tupate chochote, Vijana wengi wajifunze kupitia kwangu. mimi niliishi ili kulinda Brand ya Diamond haliyakuwa mfukoni sina kitu, niliishi ili niendane na Brand ya msanii mkubwa lakini katika nafsi yangu nilimia sana, Wakati huo sikuwa na gari wala pikipiki wala chombo chochote cha usafiri lakini nilikuwa napanda magari ya kulipi” Mwarabu aliongeza “Mshahara wangu haukutosha hata kwa wiki mbili lakini sikuwa na namna”