Staa na mrembo maarufu Gigy Money, ametoa ya moyoni kuhusu kupungua kwa muigizaji Wema Sepetu, pamoja na masuala yake ya urembo na urafiki na kinachoendelea kwenye mahusiano yake kwa sasa.


Gigy Money ameieleza EATV & EA Radio Digital, wakati wa sherehe ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa  mrembo Wema Sepetu, iliyofanyika usiku wa kuamkia Jumamosi ya September 28, 2019, katika ukumbi wa starehe uliopo Masaki Jijini Dar Es Salaam.

"Nam 'support' sana kwa sababu Mwanamke mnene hana ladha, hana swaga,unaweza kufanyiwa upasuaji ili upunguze mwili ila ni pesa yako tu, haina madhara, kwahiyo mwanamke akiwa lele mama mwili unamuelemea, hata mimi niliwahi kuwa mnene na nikapungua" amesema Gigy Money.

Aidha Gigy ameeleza nia yake ya kununua gari kabla ya huu mwaka kuisha  na kwamba yeye ndiye msanii anayevaa nywele halisi za bandia na huzivaa mara moja na akizivua huwa anazigawa kwa watu wake wa karibu.

Akizungumzia suala la mahusiano yake, Gigy amesema kwa sasa hayuko tayari kuyaweka hadharani.