Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Burna Boy amesema hataweza kwenda nchini Afrika Kusini tena hadi pale ambapo serikali ya nchi hiyo itakapomaliza sakata la raia wa kigeni kuporwa mali zao (Xenophobia).

Kupitia majibizano yake na rapa AKA kutoka South Africa kwenye mtandao wa Twitter, Msanii huyo amesema toka mwaka 2017 hajawahi kukanyaga Afrika Kusini na hataweza kuibuka tena kutokana na machafuko yanayoendelea licha yakuwa na mashabiki. wengi katika nchi hiyo.

Wasanii kibao duniani wamelaani vikali juu ya suala la Xenophobia akiwemo Chris Brown ambaye kupitia kwenye mtandao wa kijamii amechapisha ujumbe wa kulaani machafuko hayo.