MODO na mwigizaji wa Bongo Muvi, Asha Salum ‘Kidoa’ amesema hataki shobo za wadada wa mjini wanaojivalisha pete ya uchumba na kukaa kidoleni miaka 10 kwani anahofia kuwa itamtia nuksi.  Katika mahojiano maalum na Gazeti la Ijumaa, Kidoa alisema anaamini kama mwanaume anampenda mtu kamwe hawezi kumzuga na kumvalisha pete kidoleni kisha kukaa nayo zaidi ya mwaka, hiyo ni kujitia nuksi, jambo ambalo hapendi litokee kwake.

“Jamani mambo ya kutiana nuksi sitaki, naamini kama mwanaume ananipenda kweli, hawezi kuchukua muda mrefu katika uchumba bila kufunga ndoa, hiyo ya kuvaa pete ya uchumba kwa miaka kumi kisha unaachwa solemba, sitaki kabisa, bora nichine kwa mama yangu tu,” alisema Kidoa.

Stori: Imelda Mtema