Msanii asiyeishiwa na vituko Harmorapa, ameeleza sababu za kuzungumza lafudhi ya nchini Kenya na kilichomfanya aandike kuwa ana umri wa miaka 9 katika mtandao wa kijamii wa Instagram.

Harmorapa ameiambia EATV & EA Radio Digital baada ya kuchaguliwa kuwa balozi wa utalii kusini na issue ya kuongea lafudhi ya Kenya ambapo amesema,

"Mimi ni mtanzania na sikutamani kuzaliwa Kenya ila kwa sababu nimekaa miezi mingi kwa hiyo imeniathiri kidogo ila najitahidi kuongea lafudhi ya kibongo, lakini bado itakuwa ngumu kwa kuwa nina wiki moja tu tangu nirudi Kenya, labda nikae sana na watanzania ndiyo nizoee kuongea tena kiswahili cha kibongobongo".

Harmorapa ameendelea kusema kwa sasa itakuwa ngumu kuongea lafudhi ya Kiswahili kwa sababu alipokuwa Kenya ilimchukua mwezi na siku kadhaa kuongea lafudhi hiyo na ilijikuta 'automatically' bila ya kulazimishwa.

Aidha msanii huyo ameeleza sababu zilizomfanya aandike ana umri wa miaka 9 kwenye 'birthday' kwa kusema watu wanachukulia poa ila ni kweli ana miaka 9, sawa na kuku wa kizungu ndani ya wiki moja anakuwa mkubwa na unamchinja.

Pia amesema familia yao imebarikiwa kuwa na mbegu kubwa na wamezaliwa watoto watatu kwa upande wa mama yake na baba wamezaliwa watoto watano.