Dada mkuu wa Bongo Fleva Komando Lady Jay Dee, amefunguka suala la wasanii kudanga, kulinda hadhi yake, maudhi ya watu na matabaka kwa wasanii wa kike.

Akiiambia EATV & EA Radio Digital kuhusu matabaka na uchache wa wasanii wa kike amesema,

"Mimi sijaona hayo matabaka na binafsi sina tabaka na mtu, sijawahi kusikia ugomvi kati ya msichana kwa msichana sana sana 'bifu' huwa nasikia kwa waname sijasikia bifu la wanawake au labda nipo nyuma nimepitwa", ameeleza Jide.

Aidha ameeleza kilichomfanya alinde hadhi ya kuwa kwenye 'game' kwa miaka 20 kwa kujiepusha na masuala ya mahusiano, muziki na mitandao ya kijamii,

"Huyu ni mimi siigizi maisha sio kwamba najaribu kuficha kitu au najitahidi haya ndiyo maisha yangu yapo hivi, kuna vitu vingi vinakera kwa sababu kila siku kuna maudhi mapya na wapo kwa kuwakera wenzao", ameongeza.

Pia ameendelea kusema hawezi kuingilia maisha ya wanawake ambao wanadanga ili kutoboa katika maisha, kwa sababu kila mtu ana namna yake ya kuishi na huwezi jua kitu gani kilichompelekea mtu kufanya hivyo wala hawezi kumhukumu mtu hata yeye ni binadamu na ana dhambi zake.