Na Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera
Wananchi katika kata ya katoro Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wamefanikiwa kumuua Mbwa aliyekuwa na kichaa na kusababisha  kuwajeruhi kwa kuwang’ata wananchi 18 katani humo.

Akiongea na Mpekuzi blog Septemba 8, 2019 Afisa mtendaji wa kata ya katoro katika Halmashauri ya wilaya ya Bukoba  mkoani hapa Innocent Mzungu amesema kwamba  mbwa huyo  amewang’ata wananchi 18 na kufanya wanafunzi kutokwenda shule na kuamua kujifungia ndani kwa siku kadhaa wakimuogopa mbwa huyo.

Ameongeza kwamba mbwa huyo alikuwa ameisha kuwa kero katika kata hiyo na kusema kwamba alifanya madhara hayo kati ya Septemba 5 na 6 mwaka huu na kufanya idadi hiyo kuwa 18.

Bwana Mzungu amesema kuwa baada ya madhara hayo kutokea ndipo wananchi wa kijiji cha Ruhoko walipoanza kumsaka mbwa huyo na kufanikiwa kumuua na tamko likatolewa kwa kila mwananchi aliyefuga mbwa na paka kuwapeleka wanyama hao kuapatiwa chanjo Sepemba 9 mwaka huu huku watakaokiuka  tamko hilo kutozwa faini.

Tatizo la mbwa kujeruhi wananchi katika halmashauri ya wilaya ya Bukoba limekuwa sugu amabapo tukio kama ilo lilijitokeza tena mwezi uliopita katika kata ya Rukoma wilayani humo ambapo baadhi ya wananchi waling’atwa na
Mbwa mwenye kichaa jambo liliwafanya viongozi hao kukaa kwa maana ya Mwenyekiti wa halmashauri,Mkurugenzi wa Halmashauri pamoja na mkuu wa idara ya mifugo na kukubaliana kwa pamoja kuwa mbwa  ambao wanabainika kuwa na kichaa wachanjwe  na kuwa hivi karibuni madawa ya kuchanja yaliletwa na tayari zoezi la kuchanjwa kwa mbwa hao linaendelea ndani ya wilaya hiyo.

Katika hilo watendaji wa kata  wametakiwa kuhakikisha wanashirikiana na wananchi ili kufanikisha zoezi hilo na kuwa ni agizo la lazima kila mbwa kupatiwa chanjo ili kuepusha madhara katika jamii.