Baada ya Taarifa za Msiba wa Mchekeshaji wa Kike Hapa Nchini Boss Martha, Mastaa tofauti wametoa pole zao na kila Mmoja Kupitia Mitandao ya Kijamii, ameonesha ni jinsi gani ameumizwa na Msanii Martha na Kutoa Pole zake ikiwemo Kuelezea Jinsi ambavyo walimfahamu Kupitia Kazi zake na Maisha Binafsi

Mbosso Ambae ni mzazi mwenzake Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, ameelezea ni Jinsi yeye Msiba huu unakuwa Mkubwa zaidi kwake, na Kufafanua Jinsi waliwahi Kupitia Changamoto mbalimbali wakati wa Mahusiano yao, lakini Pia Kumuombea Heri na Pumziko jema kwa Mwenyezi Mungu

Kupitia Page yake ya Instagram, #Mbosso Ameandika kuwa -
Licha ya Vipingamizi Vingi juu ya Mimi kuwa na Wewe takribani au ndani ya zaidi ya Miaka Mitano (5) iliyopita, hatukuacha kuonyeshana ni kiasi gani tulikuwa tunahitajiana sana kwenye Safari yetu ya maisha , Japo jitihada zetu hazikuweza kufanikisha Mimi na wewe Kuwa Pamoja .., ila mbegu tuliyoipanda vuno letu ulichagua Liwe siri baina yangu Mimi na wewe.., sikukubishia japo Mwazoni nilikukatalia kwa sababu 'najijua kifua cha Kuficha Siri sina..' , ila nikakuahidi sitadiriki kuitoa Popote na hata waliotuhisi tulikuwa tunawakatalia.., iwe Faragha au mbele ya hadhira tulitamka Sio Kweli, Hapana, Hakuna Kitu Kama hicho..' Hayo ndo yalikuwa Majibu Yetu.., "Sasa Umeondoka bila kunipa ruksa juu ya hili Je, niendelee kuitunza hii siri .., na Je, anavyoendelea Kukua akija kuniuliza na nikwambia Mama alisema uwe siri atanielewa Kweli ''.." ?.. Wallah Moyo wangu unauma Martha , hukupaswa kuondoka wakati huu, Mapema mno Dah ..!! "Nenda Martha Mwingi Furaha na Ucheshi , Hata Mama Kasema Leo Msiba..:, ' jana ulikuwa unatabasamu hadi ulipofumba Macho , "Innalillah Wainnailaih Raajuun " ..' Mwenyezi Mungu akupe Kauli thabiti inshaallah.., ' Lala salama Martha 🙏