Wanawake wanne ambao wanajihusisha na Ukaaba na Mwanaume Mmoja ambae anadaiwa kuwa Mteja wao wamehukumiwa kifungo cha miezi sita Jela na mahakama ya mwanzo Makole, Mkoani Dodoma pamoja na kuchapwa viboko vitatu kila mmoja wakati wanaingia jela.

Hukumu hiyo inatolewa baada ya jeshi la Polisi Mkoani Dodoma kuendelea na msako wa kuwakamata Wanawake wanaodaiwa kuwa Makahaba katika maeneo mbalimbali Mkoani hapo ambao wanafanya kazi ya kuuza mili yao kama sehemu ya kujiingizia kipato.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Gilles Muruto alisema Msako wa wakina dada ambao wanauza mili yao unaendelea na kuwataka wanaofanya biashara hiyo kuacha mara moja.