Mbunge  wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu, ameonesha ni kwa namna gani ambavyo hakutegemea kama Rais Magufuli, angefurahishwa na uwepo wake kama mwakilishi wa wananchi katika jimbo hilo.

Mtaturu ameyabainisha hayo leo Septemba 17, 2019, ikiwa ni siku moja imepita tangu Rais Magufuli alipompongeza na kuiagiza Wizara ya Maji, kuhakikisha inatatua changamoto na kero ya maji  kupitia hoja aliyoiwasilisha Bungeni wakati akila kiapo siku ya Septemba 3, 2019.

''Kwahiyo nimefurahi namna ambavyo Mheshimiwa Rais amelipokea na kuelekeza Wizara ilifanyie kazi, kwahiyo mimi ntafuatilia ili kuhakikisha hiyo ahadi inatekelezwa na huduma inatolewa kwa wananchi'' amesema Mtaturu.

Aidha Mbunge Mtaturu ameongeza kuwa, licha ya uwepo wa changamoto hiyo kuzaa matunda kwa kuahidiwa itatuliwa kwa uharaka, amesema kuwa  Septemba 20 anatarajia kurudi jimboni kwake na kukutana na wananchi na kuchapa kazi kama alivyowaahidi.