China itakuwa na gwaride kubwa la kijeshi hapo kesho kwa ajili ya kusheherekea miaka 70 ya chama kinachotawala nchini humo cha 'Communist' , na nchi hiyo imehaidi kuonyesha silaha mpya zinazotengenezwa nchini humo katika mji wa Beijing.

Je, ni silaha gani watakazozionyesha na kwanini China sasa inatambuliwa kama taifa la pili lenye bajeti kubwa ya kijeshi duniani?

Uwanja mkubwa wa ndege wafunguliwa China
Kwa nini Marekani inapoteza uwezo wake wa kijeshi dhidi ya China na Urusi?
Oktoba mosi kuna mipango gani?

Gwaride la kijeshi ni miongoni mwa mambo makubwa yatakayofanyika katika sherehe hiyo kubwa itakayofanyika katika eneo la Tiananmen litahudhuriwa na maafisa wakubwa, wananchi kadhaa walioallikwa na askari 188 kutoka nchi 97.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Pamoja na shauku kubwa iliyopo miongoni mwa watu lakini ni watu wachache u ndio watapata nafasi ya kuhudhuria
Msemaji wa waziri wa ulinzi alisema hivi karibuni kuwa China haina mpango au haiitaji kuonyesha nguvu iliyonayo lakini wamelenga kuonyesha upendo, amani na namna China inawajibika.

Gwaride hili limelenga kuwavutia wengi na litatumika kuonyesha vitu.

Wizara ya uinzi imeripoti kuwa wanajeshi 15,000 watashiriki pamoja na 59 ambao watatoka vikosi mbalimbali , huku silaha 580 zitaonyeshwa katika mitaa mbalimbali na ndege za kijeshi 160 zitarushwa angani.

Rais Xi Jinping atakagua gwaride hilo katika makutano ya Chang'an mjini Beijing na baada ya hapo ndege za jeshi zitaruka katika eneo la Tiananmen.

Kwa mara ya kwanza, askari 8,000 kutoka China ambao walikuwa mashujaa wa ulinzi wa amani wa Umoja wa mataifa wataweza kushiriki.

Ni Silaha gani tutaziona?

Jeshi la 'People's Liberation Army (PLA)' lina shauku ya kuonyesha silaha mpya katika hadhara ambazo zimeshaanza kutumika.


Maadhimisho yaliyofanyika mwaka 2015
Miongoni mwa silaha ambazo zinatarajiwa kuoneshwa:

Silaha mpya ya DF-41 ambayo wachambuzi wanasema kuwa imelenga kutumika sehemu yoyote ulimwenguni itaweza kuonyeshwa.
Silaha nyingine ni MIRV ambayo ina muongozo maalumu wa ufanyaji kazi, ina uwezo wa kupiga maeneo 10 tofauti katika eneo kubwa .
Mashine nyingine ni DF-17, inatajwa kuwa gari kubwa lenye uwezo wa kubeba mzigo mkubwa na ina kasi kubwa.
Silaha nyingine mpya za magari, ndege na meli za kijeshi zitaweza kuonyeshwa.
Two unmanned aircraft Ndege mbili za kijeshi ambazo hazikutajwa majina zikiwa na muundo wa ndege isiyokuwa na rubani pia zitaonyeshwa ingawa zinalengwa kuitwa DR-8 .